Exodus 38:1-6

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

(Kutoka 27:1-8)

1 aAkatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu;
Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.
nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wa dhiraa tano
Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.
2 dAkatengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu zikawa zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. 3 eAkatengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama na vyombo vya kuchukulia moto. 4Akatengeneza wavu wa shaba chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. 5Akasubu pete za shaba za kushikilia ile mipiko kwa ajili ya zile pembe nne za huo wavu wa shaba. 6Akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuifunika kwa shaba.
Copyright information for SwhKC